https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> UBINAFSI USIVYOFAA KATIKA MAISHA

UBINAFSI USIVYOFAA KATIKA MAISHA

 ðŸ”´ TUJIFUNZE KITU HAPA 🔴


Mume alirejea kutoka kazini jioni akamwambia mke wake kuwa, “ nimewakumbuka wazazi sana, hivyo nimewaomba watutembelee kesho ”, kwa unyonge mke akaitia “ sawa ”.

Asubuhi mapema mume akaamka kujiandaa ili aende kazini, akamkumbusha mkewe kuwa, “ fanya maandalizi mazuri kwa ajili ya chakula na vinywaji, naenda kazini nitarudi mchana ili kuwapokea wazazi.” Mume akaondoka, mkewe anaendelea kulala.


Mume akarudi mchana akakuta hakuna maandalizi yoyote, akamuuliza mkewe “ mbona haujafanya nilivyokuagiza ?”, mke akajibu “ wakija watakula chochote watakachokikuta ”.

Mume akaondoka kwa hasira, muda mfupi mke akasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua akastaajabu kukuta ni baba na mama  yake, na mdogo wake wa kiume, baba yake akauliza; “ mkwe yuko wapi maana yeye ndiye aliyetualika ”.

Mke akaingia chumbani akiwa na furaha akachukua simu akampigia mumewe na kumuuliza “ uko wapi mume wangu, maana baba, mama, na mdogo wangu wamefika, hivyo naomba upitie sokoni ununue nyama, kuku, na matunda ”.  Mume akamwambia “ hakuna haja ya vitu vyote hivyo, watakula chochote kilichopo kama ulivyosema ”.


🔴 Mpaka hapo, tunajifunza kuwa ubinafsi sio mzuri katika mahusiano na maisha kiujumla.

Tambua kwamba, wazazi wote ni wa muhimu, iwe ni wa upande wa mume au mke.🔴


✍️👷 Visit our social media, Facebook & Instagram @Patrick Manuma 

Electrical Technician / Fundi Umeme

Blogger / Mwanablogu

Diagrams Designer / Mbunifu wa Michoro na Ramani.




Post a Comment

0 Comments