https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> KARIAKOO DERBY, SIMBA SC vs YOUNG AFRICANS SC.

KARIAKOO DERBY, SIMBA SC vs YOUNG AFRICANS SC.

Mchezo wa watani wa jadi wa ligi kuu ya NBC nchini Tanzania, uliochezwa kati ya timu ya Simba SC na timu ya Yanga SC. Ikiwa ni siku ya Jumapili ya tarehe 05/11/2023, kwenye uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa, Daresalam. Matokeo ya mtanange huo yaliipa Yanga ushindi wa goli 5 kwa 1,
ushindi ambao umeifanya nchi kuzizima kwa shangwe upande wa mashabiki wa Yanga, huku ikiwa ni simanzi kwa mashabiki wa Simba. Kufuatia matokeo hayo, timu ya Simba SC imefikia makubaliano ya pande zote na kuvunja mkataba wa kocha wao mkuu Robertino.
Kwa muda huu wa mpito, timu imebaki chini ya aliyekuwa kocha wa viungo, mbrazili Daniel Cadena
na kocha msaidizi Selemani Matola.
Ratiba nyingine za ligi kuu Tanzania zilizoendelea siku ya jana tarehe 08/11/2023, timu ya Yanga ilivaana na timu ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani, mkoani Tanga. Ambapo timu ya Yanga ilitoka na ushindi wa goli 1 kwa 0.
Pia leo tarehe 09/11/2023 kumeshuhudiwa mtanange mkali kati ya timu ya Simba SC dhidi ya timu ya Namungo FC, huku matokeo yakiwa ni sare ya goli 1 kwa 1.
Kwa sasa msimamo wa ligi kuu ya NBC Tanzania, unaongozwa na Yanga SC.

#KARIAKOO_DERBY #NBCFremierLeague

Sponsored by: @ManumaElectricalWorks , (official FB and IG pages).

Post a Comment

0 Comments