https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> MAPIGANO KATI YA URUSI NA UKRAINE

MAPIGANO KATI YA URUSI NA UKRAINE

Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ulianza mnamo Februari 2014,chanzo kikiwa ni kutaka kujitenga kwa vikosi vinavyosaidiwa na kila upande miongoni mwa mahasimu hao.
Mzozo huo ukazuka tena kuanzia 2021 hadi 2022,ni baada ya kudhihirika wazi nia ya Urusi ikitaka kuanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya Ukraine ilipofika Februari 2022. Mazungumzo ya kidipromasia yamefanyika lakini yalishindwa vikali na Urusi ikashikilia msimamo wake kwa kupeleka wanajeshi kwenye maeneo wanayotaka kujitenga mnamo Febuari 22 2022. Ilipofika Februari 24 Urusi ikaanzisha uvamizi kamili dhidi ya Ukraine,ambapo mpaka sasa mapigano hayo yameleta athari kwa raia. Raia wa nchi hizo na raia wageni kutoka nchi mbalimbali wamekwama kuondoka baada ya njia za usafiri kuharibika,hatua hiyo ikitanguliwa na njia za anga kufungwa.
Awali raia wa kigeni walizuiliwa kutoka nchini Ukraine kwenda mipakani ili kupata msaada wa kwenda kwenye nchi zao,mpaka kufika jana Machi 9 ambapo Ukraine ilitangaza kuwa imekubaliana na Urusi kusitisha mapigano hayo ili kuruhusu raia kutoka na kwenda sehemu salama kupata hifadhi.
Mchambuzi mmoja amesema kuwa kila mtu duniani ana wajibu wa kuiombea Urusi na Ukraine ili hatimaye wamalize mapigano hayo,https://business.fiverr.com/share/gE4YaA maana licha ya madhara kwa raia wao na wageni,madhara yanaweza kwenda dunia nzima kiuchumi kutokana na bidhaa kama mafuta kupanda bei kwa sababu ya kushuka kwa uzalishaji wake kwenye nchi hizo.

Post a Comment

0 Comments