https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> SERIKALI YATUPIA JICHO KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA.

SERIKALI YATUPIA JICHO KUPANDA KWA BEI YA BIDHAA.

Serikali ya Tanzania imeamua kudhibiti suala la kupanda kwa bei za bidhaa zingine,kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya Petroli na Dizeli kwenye soko la dunia. Hatua hiyo imekuja baada ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara,kufanya mkutano na waandishi wa habari leo hii tarehe 11/04/2022 katika ukumbi wa Hazina,Dar-Es-Salam.
Katika kufungua mkutano huo uliohusisha pia sekta binafsi na wenye viwanda,Waziri wa Viwanda na Biashara,Dkt.Ashatu Kijaji amesema katika kukabiliana na kupanda kwa bei za bidhaa,Serikali inazungumza na wenye viwanda ili kutokupandisha bei ya bidhaa wanazozalisha. Pia Serikali inakusudia kupunguza ama kuondoa kabisa baadhi ya tozo hasa katika sukari na mafuta ya kula,ili kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi.
Suala lingine ni kupunguza na kudhibiti bei za vifaa vya ujenzi sokoni,hasa nondo na simenti kwa kuweka uwiano mzuri kati ya bei ya kiwandani isipishane mbali na bei ya sokoni licha ya gharama za usafirishaji kutokana na kupanda bei kwa mafuta ya Petroli na Dizeli.
Baadae Waziri wa Fedha na Mipango,Mh.Mwigulu Nchemba alizungumzia hali halisi ya kiuchumi kwa nchi na namna Serikali inavyochukua hatua kuzuia upandishaji holela wa bei za bidhaa.Pia ameeleza namna Serikali ilivyopambana na hali ya uchumi wakati janga la Corona,ukuaji kiuchumi wa sasa wa asilimia 4.2 na matarajio ya Serikali kuendelea kukuza hali ya uchumi nchini hadi kufikia asilimia 5.5.
Awali Dkt.Kijaji alielezea sababu za kupanda kwa bei za bidhaa hapa Tanzania na nchi nyingine za Afrika na dunia kwa ujumla,ambapo amesema vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine ni sababu moja wapo.Na sababu nyingine ni majanga yaliyoikumba dunia toka mwaka 2019 ya UVIKO 19 (Corona),ambapo janga hili lilitikisa nchi nyingi na kupelekea uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa kupungua. Nchi nyingi ikiwemo Tanzania zinanunua bidhaa nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya walaji,mfano wa bidhaa kama mafuta ya magari,na ngano Serikali inanunua kwa kiasi kikubwa kutoka Urusi. Karibia asilimia 88 (tani 8) ya ngano inayohitajika hapa nchini inanunuliwa Urusi,ni asilimia 12 tu (tani 1) ya ngano yote ndiyo inalimwa hapa nchi. Hivyo madhara ya mgogoro kati ya Urusi na Ukraine yanatukumba pia kama nyingi nyingine duniani zinazotegemea bidhaa kutoka kwa nchi hizo,kwa sababu Tanzania sio kisiwa kwamba isikutwe na athari hizo ikiwemo kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu ya mafuta katika soko la dunia.

Post a Comment

0 Comments