https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> SIMBA SC vs ORLANDO PIRATES

SIMBA SC vs ORLANDO PIRATES

Timu ya Simba ambao ni wawakilishi pekee Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Ubingwa wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF),Jumapili hii ya tarehe 17 April 2022 watakuwa wenyeji dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali katika uwanja wa taifa,Benjamin Mkapa National Stadium.
Kabla ya hatua hii ya robo fainali Simba SC ilikutana na timu kadhaa katika hatua ya makundi,zikiwemo RS Berkane,na USG,ambapo kuna michezo alifungwa,mingine alishinda hasa nyumbani,na mingine akatoka sare.
Kumbuka,kwa mara ya kwanza barani Afrika CAF inatarajia kutumia mfumo wa VAR (Video Assistant Refaree),katika mechi hiyo ambayo timu ya Simba inatakiwa kushinda magori mengi ili kutengeneza njia rahisi katika hatua inayofuata,ambapo baada ya wiki moja mchezo utarudiwa huku Orlando Pirates wakiwa nyumbani(Afrika Kusini
Pamoja na yote bado Simba ana sababu ya kushinda kwa kutokana na maandalizi yanayoendelea kufanyika,kwanza timu yenyewe imejipanga vilivyo kuanzia Kocha Pablo na kikosi chake.Pili,benchi la ufundi linabuni hamasa tofauti tofauti ili kuleta radha ya mechi,tatu na mwisho ni mashabiki takribani elfu sitini (60,000) walioruhusiiwa na CAF kuingia uwanjani wataleta hamasa kubwa.

Post a Comment

0 Comments