https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> MAUNDA ZORRO AFARIKI KWA AJALI

MAUNDA ZORRO AFARIKI KWA AJALI

Mwanamuziki wa siku nyingi wa miondoko ya Zouk/RnB Tanzania,Maunda Zahir Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Alhamisi tarehe 14,April 2022. Taarifa za kutokea kwa msiba huo zimethibitishwa na kaka wa marehemu,ambaye naye pia ni mkongwe wa Bongofleva Banana Zahir Zorro.
Banana Zorro amesema alikuwa na mdogo wake kwenye msiba wa rafiki yao jana,ambapo yeye aliondoka saa 12 jioni akamuacha mdogo wake na ilipofika saa nne Maunda Zorro alikuwa barabarani anarudi nyumbani kwake Kigamboni. Inasemekana ajali ilisababishwa na kugongana kati ya gari ndogo aliyokuwa anaendesha na lori lililokuwa limebeba mchanga,marehemu ameacha watoto watatu na msiba upo nyumbani kwa mzee Zahir Ally Zorrro,Maweni Kigamboni. Banana Zorro na marehemu mdogo wake Maunda Zorro wamezaliwa kwenye familia ya muziki,kutoka kwa baba yao mwanamuziki nguli na wa siku nyingi mzee Zahir Ally Zorro.
Mwanadada huyo amewahi tamba na vigongo kadhaa katika maisha yake ya muziki,miongoni mwa nyimbo hizo ni “Mapenzi ni ya wawili” na “Nataka niwe wako” ambazo ziligonga vichwa vya wapenzi wa muziki miaka hiyo ya 2005-2010. Rest In Peace Maunda.

Post a Comment

0 Comments