https://srv.adstxtmanager.com/2147483647/nwanajamiitanzania.blogspot.com'); exit; ?> ORLANDO PIRATES vs SIMBA SC

ORLANDO PIRATES vs SIMBA SC

Leo Jumapili tarehe 24 April 2022 kutashuhudiwa mtanange mkali wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF),kati ya Orlando Pirates ya Afika Kusini dhidi ya Simba SC ya Tanzania.
Mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Orlando Stadium uliopo Soweto,Afrika Kusini,ikiwa ni hatua ya pili baada ya ile ya kwanza kufanyika Tanzania kwenye uwanja wa Mkapa tarehe 17 April na Simba kupata goli moja kwa mkwaju wa penati.
Jana Jumamosi Simba imefanya maandalizi kadhaa huko Johannesburg, Afrika Kusini,ambapo wachezaji wa Simba walifanya mazoezi ili kujiweka sawa na tayari kukabiliana na mchezo wa leo.
Pia wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Simba walifanya mazungumzo na Rais wa heshima na mwekezaji wake @MooDewji kupitia mtandao (online video Conference),ili kuweka mikakati ya kupata ushindi kwenye mechi hiyo.
Mashabiki pamoja na wachambuzi wanaitabiria ushindi @SimbaSCTanzania kwa kuwa itaingia ikiwa na goli moja,hivyo wanaiombea njaa @OrlandoPirates ili Simba ishinde ama kutoka na sare yoyote. Ikiwa timu ya Simba ikishinda mchezo huu wa leo itapanda hatua na kuingia nusu fainali,klabu ya Simba ndio wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano hayo yanayohusisha vilabu Afrika. Kila la heri @SimbaSCTanzania.

Post a Comment

0 Comments